Rais wa Tanzania anaungana na viongozi wa kimataifa kumpongeza Xi
2023-03-15 15:03:47| cri

Rais Samia Suluhu Hassan ameungana na viongozi wengine duniani kumpongeza Rais Xi Jinping wa China kwa kuchaguliwa tena katika muhula wa tatu. Katika ujumbe wake wa pongezi kupitia akaunti yake rasmi ya twitter, Mama Samia alimuahidi Xi kuimarisha uhusiano na China.

"Natarajia kuendelea kushirikiana pamoja ili kuimarisha ushirikiano wa kina wa kimkakati kati ya Tanzania na China," inasomeka sehemu ya ujumbe wa Rais Samia.

Kwa mujibu wa News24, wakuu wengine wa nchi za Afrika ambao wamempongeza Rais Xi wa China ni pamoja na rais William Ruto wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe n.k.

Wiki iliyopita, Xi Jinping alichaguliwa kwa kauli moja kuwa Rais wa China. Pia alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi kwa kura zote.