Baraza jipya la Serikali ya la China laanza kutekeleza majukumu
2023-03-15 08:57:00| CRI

Baraza jipya la Serikali la China limeanza rasmi kutekeleza majukumu kufuatia Waziri Mkuu Li Qiang kuendesha mkutano wa kwanza wa baraza hilo jana Jumanne.

Mkutano huo ulipitia kazi zinazohusiana na uundaji wa baraza hilo na kujadili kanuni za kazi za baraza hilo zilizorekebishwa upya.

Kuhusu mageuzi ya kitaasisi ya baraza hilo, mkutano huo umesema yanapaswa kuchukuliwa kama fursa ya kuleta mabadiliko kwenye kazi za serikali, kuelekea mahitaji ya kuhimiza njia mpya ya maendeleo, na kuchochea maendeleo yenye ubora wa juu nchini China.