Mpiga gitaa maarufu wa Kongo, Denis Lokassa Kasiya, almaarufu Lokassa ya Mbongo, alifariki Jumanne usiku nchini Marekani baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Lokassa, ambaye hivi majuzi alifikisha umri wa miaka 80, alikuwa kiongozi wa bendi maarufu ya Soukous Stars, iliyokuwa na makao yake mjini Paris. Awali, aliwahi kutamba na bendi ya Tabu Ley Rochereau's Afrisa International na baadaye bendi ya All African Stars. Alikuwa akipambana na ugonjwa wa kisukari na alikuwa akijiuguza kutokana na kiharusi kidogo alichopata miaka michache iliyopita.
Mwanamuziki mwenzake wa Kongo anayeishi Marekani, Mekanisi Modero alisema alikuwa na matatizo ya kupumua kabla ya kuzimia na kufa huko Nashua, New Hamsphire.