Watu 87 Tanzania hufariki kwa TB kila siku
2023-03-16 22:01:53| cri

Ugonjwa wa Kifua Kikuu au TB ni janga linaloua kimya kimya ambapo takwimu zinaonesha kuwa Tanzania watu 87 hupoteza maisha kila siku kutokana na ugonjwa huo na kuifanya kuwa miongoni mwa nchi 30 duniani zenye maambukizi makubwa ya TB.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma jijini Dar es Salaam, Dokta Mbarouk Seif Khaleif amesema Tanzania kila mwaka watu 137,000 huugua TB na husababisha vifo 32,000, sawa na vifo 87 kila siku kati ya vifo hivyo, 33 ni vya waliokuwa wanaishi na virusi vya ukimwi (WAVIU).

Naye Mratibu wa TB wilaya ya TB Mnazi mmoja Dokta Linda Mutasa amesema kumekuwa na dhana potofu kuwa mwenye kifua kikuu lazima awe na ukimwi au amerithi na wengine kwenda mbali na kudai kuwa wamerogwa.