Mjumbe wa China anayeshughulikia maswala ya Pembe ya Afrika Balozi Xue Bing, amesema China inaunga mkono juhudi za serikali ya Ethiopia na watu wake kufikia amani ya taifa, umoja na maendeleo.
Balozi Xue Bing amesema hayo wakati akiongea na wanahabari, na kusema huduma za kimsingi za umma na misaada ya kibinadamu imeanza kurudishwa polepole, na serikali ya mpito ya eneo la Tigray imekuwa na maendeleo chanya.
Amesema China inaamini kuwa mgogoro wa Tigray ni jambo la ndani la Ethiopia na linatakiwa kutatuliwa na waethiopia wenyewe kwa njia ya mazungumzo, na kusisitiza kuwa maendeleo ya kupatikana kwa amani nchini Ethiopia yanaonesha kuwa watu wa Ethiopia wana busara na uwezo wa kutatua changamoto za ndani wao wenyewe kwa njia ya mazungumzo.