Baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika wametoa pongezi kwa njia ya simu na barua kwa Bw. Xi Jinping kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Watu wa China.
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amepongeza Bw. Xi kwa kuchaguliwa tena kuwa rais, huku akisema anapenda kushirikiana na rais Xi kuimarisha uhusiano wa pande zote wa kimkakati na kiwenzi kati ya Tanzania na China.
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC amesema anapenda kushirikiana na rais Xi kwa moyo wa uwazi na ushirikiano wa kunufaishana, ili kuimarisha na kuendeleza urafiki wa jadi kati ya DRC na China ambao umedumu kwa zaidi ya nusu ya karne na kujenga mustakabali mzuri zaidi kwa pande mbili.
Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon amesema ana imani kuwa uamuzi uliofanywa na mikutano miwili ya China utaharakisha mchakato wa kisasa wa China, na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa China. Pia amesema anapenda kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Gabon na China.
Viongozi wengine akiwemo rais Alassane Ouattara wa Cote d'Ivoire, rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Guinea ya Ikweta, na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pia wametoa pongezi kwa rais Xi kuchaguliwa tena kuwa Rais.