Rais Xi ahimiza vyama vya kisiasa viweke dira kuelekea ujenzi wa nchi ya kisasa na kutoa Pendekezo la Ustaarabu Duniani
2023-03-16 08:49:11| CRI

Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ametoa wito kwa vyama vya kisiasa duniani kuunganisha kwa karibu maendeleo yao na msukumo wa kuzijenga nchi zao kuwa za kisasa, ili kuendelea kuongoza njia na kukusanya nguvu kwa ajili ya ujenzi wa nchi ya kisasa.

Rais Xi ametoa kauli hiyo jana Jumatano alipohutubia kwa njia ya video ufunguzi wa Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Mazungumzo kati ya CPC na Vyama vya Kisiasa Duniani.

Kwenye hotuba yake Rais Xi pia ametoa Pendekezo la Ustaarabu Duniani, ambapo ametoa wito wa kuheshimu anuwai ya staarabu, kulinda maadili ya pamoja ya ubinadamu, kuthamini urithi na uvumbuzi wa staarabu, na kuhimiza kwa pamoja mawasiliano kati ya watu na ushirikiano wa kimataifa.