China yatoa mpango wa mageuzi katika taasisi za Chama na serikali
2023-03-17 13:16:16| cri

Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Baraza la Serikali wametoa mpango wa mageuzi katika taasisi za Chama na serikali, na kutoa waraka wa kutaka mpango huo utekelezwe kwa uaminifu.

Kwa mujibu wa mpango huo, tangu kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC, juhudi zinaendelea kufanywa ili kurekebisha zaidi taasisi za Chama na serikali, na kupelekea mabadiliko ya kimfumo na ya jumla ya kazi zao. Hata hivyo, mpangilio wa taasisi na ugawaji wa majukumu ya taasisi za Chama na serikali bado haujatumiwa kikamilifu kwenye kazi mpya, na kwamba mageuzi na marekebisho yanahitajika zaidi.

Mpango huo unaendelea kufafanua kuwa lengo la kurekebisha taasisi za Chama na serikali ni kujenga mfumo wa kiutendaji wa taasisi za Chama na serikali ulio bora zaidi, unaozingatia utaratibu na ufanisi. Aidha mipango muhimu iliwekwa katika Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC kwa ajili ya kuimarisha mageuzi ya taasisi za Chama na serikali, ambayo ina umuhimu mkubwa.