Tanzania yaahidi kufanya mageuzi ya elimu ya juu ili kuchochea maendeleo ya uchumi
2023-03-17 21:02:19| cri

Mamlaka nchini Tanzania zimeahidi kufanya mageuzi ya elimu ya juu ili kuiwezesha kuchukua nafsi yake katika ukarabati wa maendeleo ya uchumi.

Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa Ufadhili kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu uliofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini humo Adolph Mkenda amesema, ili kufikia lengo hilo, serikali itaendelea kutoa ufadhili kwa elimu ya juu. Amesema kuanzia mwaka 1994 mpaka sasa, serikali imetoa mikopo kwa elimi ya juu inayofikia dola za kimarekani bilioni 2.3 kwa wanafunzi 654,919. Amewataka wadau katika sekta ya elimu kutafiti mbinu za kupata vyanzo mbadala vya ufadhili kwa wanafunzi wa elimu ya juu.