Kwenye Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Mazungumzo kati ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na Vyama vya Kisiasa Duniani uliofanyika tarehe 15 Machi, rais wa China Xi Jinping alitoa fikra yake mpya ya kuhimiza jamii ya kisasa ya binadamu na Pendekezo la Ustaarabu Duniani.
Xi alitoa mapendekezo matano juu ya mambo ya kisasa, ambayo ni kuweka kipaumbele kwenye maslahi ya wananchi katika mwelekeo wa kisasa, njia za aina mbalimbali za kutafuta mambo ya kisasa, mchakato endelevu, matokeo yanayonufaisha watu wote duniani na uongozi imara. Kutoa kipaumbele kwenye maslahi ya wananchi ni wazo kuu la Xi Jinping katika utawala wa nchi. Matokeo yanayonufaisha watu wote duniani ni wazo la jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja lililotolewa na Xi Jinping. Kwenye mkutano huo, Xi alifafanua tena maendeleo ya kisasa ya China, fikra ambayo inaonyesha wazo lake katika utawala wa nchi.
Xi pia alitoa Pendekezo la Ustaarabu Duniani kwa mara ya kwanza, ambapo ametoa wito wa kuheshimu ustaarabu anuwai, kulinda maadili ya pamoja ya binadamu, kuthamini urithi na uvumbuzi wa ustaarabu, na kuhimiza kwa pamoja mawasiliano kati ya watu na ushirikiano wa kimataifa. Xi alisema ustaarabu tofauti kuishi pamoja kwa masikilizano, kuwasiliana na kufunzana, vinafanya kazi muhimu katika kuhimiza mchakato wa jamii ya kisasa ya binadamu na kustawisha usataarabu wa dunia.
Njia ya China kujiendeleza ikiwa ni mtindo mpya wa ustaarabu wa binadamu, inafundishana na ustaarabu wa maeneo mengine mbalimbali duniani, hali ambayo itastawisha zaidi ustaarabu wa dunia.