China iko tayari kuisaidia Pembe ya Afrika kuwa eneo lenye amani, ushirikiano na maendeleo ya pamoja
2023-03-17 08:45:56| CRI

Mjumbe maalumu wa China anayeshughulikia suala la Pembe ya Afrika Balozi Xue Bing ambaye yuko ziarani nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika, amesema China iko tayari kuisaidia pembe ya Afrika kuwa eneo lenye amani, ushirikiano na maendeleo ya pa moja.

 Wakati huo huo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Bw. Blinken pia yuko ziarani nchini Ethiopia. Kuhusiana na jinsi China inavyozingatia ushirikiano kati ya nchi mbalimbali na Ethiopia, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bw.Wang Wenbin amesema kwamba nchi zote zinapaswa kuchukua hatua halisi za kivitendo zinazofaa kwa maendeleo ya Ethiopia na amani ya kikanda, badala ya kuweka vikwazo au kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa kisingizio cha masuala yanayofuatiliwa na pande mbalimbali.

Bw. Wang Wenbin ameeleza kuwa moja ya kazi muhimu za ziara ya mjumbe huyo maalum nchini Ethiopia ni kudumisha mawasiliano ya karibu na nchi za eneo hilo ili kuhimiza utekelezaji wa Amani na Maendeleo katika Pembe ya Afrika na kusaidia nchi katika kanda kutimiza umoja, kujiendeleza, ustawi na utulivu. Amesema China pia inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuisaidia Ethiopia kuwa na amani, ushirikiano na maendeleo ya pamoja.