Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi na Fedha ya Afrika ya Kati (CEMAC) wamerejea tena ahadi yao ya kuongeza kasi ya maingiliano ya kikanda na kuchochea ukuaji.
Viongozi hao wametoa ahadi hiyo katika Mkutano wa 15 wa CEMAC uliofanyika katika mji mkuu wa Cameroon, Yaounde.
Kwa mujibu wa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo, zaidi ya dola za kimarekani bilioni 2 zitasambazwa kufadhili miradi ya maingiliano katika kanda hiyo. Viongozi hao pia walipitisha mageuzi yatakayosaidia kuimarisha maingiliano ya kikanda, kuboresha uchumi wa nchi wanachama kufuatia athari zilizotokana na janga la COVID-19 na mgogoro kati ya Russia na Ukraine, na pia kuimarisha uhusiano wa kiusalama.