China yatoa ripoti kuhusu hali ya demokrasia ya mwaka 2022 nchini Marekani
2023-03-20 14:21:50| CRI

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetoa ripoti kuhusu hali ya demokrasia ya mwaka 2022 nchini Marekani.

Ripoti hiyo inasema, mwaka 2022, Marekani imeendelea kutumbukia katika mzunguko mbaya wa upotoshaji wa kidemokrasia, udhaifu wa kisiasa, na ukosefu wa masikilizano ya kijamii, na kukabiliwa na matatizo kama vile siasa za kifedha na kiwadhifa, migongano ya kijamii, na pengo kati ya watu matajiri na maskini. Licha ya matatizo yake yenyewe, Marekani bado inanyooshea vidole mambo ya ndani ya nchi nyingine na kupenda kuwa mwalimu wa demokrasia.