Kenya yapiga marufuku maandamano makubwa yaliyoandaliwa na wapinzani
2023-03-20 09:54:55| CRI

Idara ya Polisi ya Kitaifa nchini Kenya imepiga marufuku maandamano makubwa yaliyoandaliwa na Muungano wa Azimio la Umoja leo Jumatatu mjini Nairobi, ambayo yanapinga kupanda kwa gharama za maisha na kukosekana kwa haki katika uchaguzi.

Akitoa tangazo la katazo, Kamanda wa Polisi wa Nairobi Bw. Adamson Bungei amesema maandamano hayo yanapigwa marufuku kwani yanaweza kuhatarisha amani na kutatiza shughuli za kiuchumi. Maandamano ya kuishinikiza serikali kukabiliana na shinikizo la mfumuko wa bei linalowakabili wananchi pamoja na kufanya mageuzi ya uchaguzi yameshindwa kukidhi matakwa ya katiba.

Amebainisha kuwa maafisa wa usalama wataongeza umakini Jumatatu ili kuepusha uvunjaji wa sheria na utaratibu huku muungano wa upinzani ukuishinikiza serikali kukabiliana na mdororo wa uchumi ambao umesababisha ukosefu wa ajira na mfumuko wa bei.