UNECA: COVID-19 na mzozo wa Ukraine yatatiza maendeleo ya Afrika
2023-03-20 09:55:52| CRI

Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) imesema madhara makubwa ya janga la COVID-19 na mzozo wa Ukraine yamezuia maendeleo ya Afrika katika sekta mbalimbali.

Taarifa iliyotolewa katika mkutano wa mawaziri wa fedha, mipango na maendeleo ya uchumi wa Afrika wa UNECA inasema, athari mbaya za janga la COVID-19 na mzozo wa Ukraine kwenye uzalishaji, biashara, na sekta nyingi za kiuchumi na kijamii zimezuia maendeleo ya Afrika.

Taarifa hiyo inasisitiza kuwa ingawa masuala ya uzalishaji, kilimo, usalama wa chakula, biashara, utawala bora na maendeleo yamezingatiwa zaidi, lakini nchi nyingi za Afrika zilizoko nyuma kimaendeleo, zimepiga hatua kidogo katika kubadilisha muundo wa uchumi ili kupata maendeleo endelevu.