Bunge la Afrika Kusini limesema, rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa atapeleka wanajeshi 3,474 tangu Machi 17 hadi April 17 ili kudumisha Amani nchini humo.
Katika taarifa yake, Bunge hilo limesema kuwa limearifiwa na rais kuhusu kupelekwa kwa Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi la nchi hiyo, kwa lengo la kuzuia na kukabiliana na uhalifu na pia kudumisha amani.
Bunge hilo limesema, kupelekwa kwa askari hao kunaendana na Katiba ya Afrika Kusini, na kiasi cha dola za kimarekani milioni 8.99 zinatarajiwa kutumika katika zoezi hilo.
Wakati huohuo, chama cha upinzani nchini humo, Wapiganaji wa Uhuru wa Uchumi wametoa wito wa kufanyika kwa maandamano ya nchi nzima hii leo ili kumlazimisha rais Ramaphosa kujiuzulu.