Galoni 400,000 za maji yenye mionzi zavuja kwenye kinu cha nyuklia cha Marekani
2023-03-20 09:59:06| CRI

Takriban lita 400,000 za maji yenye mionzi zimevuja kwenye kinu cha nuvu za nyuklia huko Monticello, jimbo la Minnesota lililopo katikati ya Marekani.

Shirika la Kudhibiti Uchafuzi la Minnesota (MPCA) lilisema kwamba mashirika ya serikali yanafuatilia juhudi za Xcel Energy za kusafisha maji yanayotolewa ambayo yamechafuliwa na tritium, iliyogunduliwa katika kiwanda cha kuzalisha nyuklia cha Monticello cha kampuni hiyo. Xcel Energy iliripoti uvujaji huo kwa Afisa Mhusika wa Minnesota na Tume ya Udhibiti wa Nyuklia ya Marekani mwishoni mwa Novemba 2022 baada ya kugundua matokeo yasiyo ya kawaida wakati wa ufuatiliaji wa kawaida wa maji chini ya ardhi.

Ucheleweshaji wa miezi minne wa kuweka hadharani uvujaji wa maji ya mionzi umezua wasiwasi kuhusu usalama wa umma na uwazi.