Operesheni ya kijeshi ya pamoja ya Uganda na DRC yapiga hatua kubwa
2023-03-20 09:58:01| cri


 

Jeshi la Uganda jana lilisema, operesheni yake ya kijeshi iliyofanywa kwa pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) dhidi ya waasi wa ADF imepata hatua kubwa.

Naibu msemaji wa jeshi la Uganda Deo Akiiki amesemakambi kadhaa za waasi huko Mashariki mwa DRC zimeteketezwa, na waasi wamekumbwa na taharuki wakikikimbia kwenye vikundi vidogo.

Majeshi ya Uganda na DRC yalianzisha mashambulizi ya pamoja dhidi ya waasi wa ADF mwezi Novemba mwaka 2022.