Wanariadha wa Afrika watawala mbio za Los Angeles Marathon 2023
2023-03-21 19:25:32| cri

Wanariadha wa Afrika wameonyesha umahiri wao katika mbio za Los Angeles Marathon za mwaka 2023, huku Jemal Yimer wa Ethiopia na Mkenya Stacy Ndiwa wakitwaa ushindi katika mbio za wanaume na wanawake. Zaidi ya wakimbiaji 20,000 walishiriki kwenye mbio hizo.

Yimer alimaliza mbio hizo za kilomita 42.16 kwa muda wa saa mbili, dakika 13 na sekunde 13.58, akifuatiwa na Yemane Tsegay wa Ethiopia na Barnaba Kipkoech wa Kenya. Ndiwa alishinda kitengo cha wanawake kwa kutumia muda wa 2:31:0.24, akifuatiwa na wanariadha wenzake wa Kenya Martha Akeno na Grace Kahura.

Mbio hizo zilianza katika Uwanja wa Dodgers mjini Los Angeles, na kumalizia kwenye Mtaa wa Nyota.