China yasema ni Marekani inayotoa silaha kwenye medani ya vita ya Ukraine
2023-03-21 09:06:16| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema ni Marekani na sio China inayotoa silaha kwenye medani ya vita ya Ukraine, na kwamba China siku zote inasimama upande wa amani na mazungumzo.

Akiongea na wanahabari Bw. Wang amesema China itaendelea kubeba jukumu la kiujenzi kwenye usuluhishi wa kisiasa wa mgogoro wa Ukraine. Pia ameitaka Marekani kutochochea moto, na kuacha kuzilazimisha na kuzitisha nchi nyingine.