Mashirika ya Utangazaji ya China na Russia kushirikiana katika matumizi ya video na picha za kihisitoria
2023-03-21 21:10:52| CRI

Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na Shirika la Radio na Televisheni la Taifa la Russia (VGTRK) leo Machi 21 huko Moscow wamesaini hati ya maelewano wakikubaliana kuimarisha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya wakuu wa nchi hizo mbili, na kusukuma mbele ushirikiano kwa pande zote, kwenye ngazi zote na katika nyanja zote. CMG na VGTRK wamekubaliana kushirikiana katika utumiaji, ukarabati na uhifadhi wa video na picha za kihisitoria za nchi hizo mbili.

Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong na mkuu wa VGTRK Bw. Oleg Dobrodeev wamesaini makubaliano hayo kwa niaba ya mashirika hayo mawili.