Watu 21 wauawa katika mashambulio ya karibuni ya waasi mashariki mwa DRC
2023-03-21 22:23:47| cri

Naibu Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema, watu 21 wameuawa katika mashambulio yaliyofanywa na waasi katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Akizungumza hapo jana, Bw. Haq amesema, katika wiki mbili zilizopita, mashambulio yaliyofanywa na waasi wa kundi la ADF yalisababisha vifo vya raia 118. Ameongeza kuwa, Tume ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) imeripoti mfululizo wa mashambulio katika mkoa wa jirani wa Kivu Kaskazini na Ituri usiku wa jumamosi, na kusababisha watu kadhaa kukimbia makazi yao.