Raia 21 wauawa kwenye mashambulizi yaliyofanywa na waasi mashariki mwa DRC
2023-03-21 09:05:33| CRI

Raia 21 wameuawa baada ya waasi kufanya mashambulizi huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wikiendi iliyopita.

Kwa mujibu wa Farhan Haq, Naibu Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, katika wiki mbili zilizopita mashambulizi ya waasi wa ADF yamesababisha majeruhi ya raia 118, ambapo Tume ya Kulinda Amani nchini DRC (MONUSCO) imeripoti mashambulizi katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri usiku wa Jumamosi, na kupelekea watu kuyakimbia makazi yao.

Bw. Haq amesema MONUSCO na vikosi vya ulinzi vya DRC vimeanza doria ya pamoja kwenye barabara ya Beni-Butembo na kushirikiana na mamlaka na jamii za huko kwenye maeneo waliyopo ADF.