Kaimu Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) Antonio Pedro amezitaka serikali za nchi za Afrika kutekeleza na kuwekeza katika mikakati inayolenga watu ili kukusanya rasilimali na kuongeza kasi ya ufufukaji wa uchumi wa bara hilo.
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha 55 cha ngazi ya mawaziri cha Mkutano wa Kamati ya Uchumi wa Afrika wa Mawaziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi uliofanyika jumatatu, Pedro amesema Afrika iko katika kiini cha mageuzi endelevu ya dunia, kama miundombinu ya usafiri wa umeme, na matumizi ya kasi ya nishati safi, mambo ambayo yanapaswa kuimarisha ufufukaji wa bara hilo kutokana na changamoto mbalimbali.
Amesisitiza kuwa Afrika inahitaji mfumo wa maendeleo unaowalenga watu ambao unajumuisha kuondokana na umasikini na usawa wa jinsia katika mikakati ya kitaifa na kikanda.