Polisi wa Afrika Kusini wana usalama nchini humo wamewakamata waandamanaji zaidi ya 550 kutokana na kufanya ghasia, vitisho, uharibifu wa miundombinu, wizi, na majaribio ya uporaji wakati wa maandamano ya nchi nzima yenye lengo kusimamisha shughuli za nchi nzima.
Taarifa iliyotolewa na polisi imesema watu 149 walikamatwa katika jimbo la Gauteng, watu 95 katika jimbo la Northern Cape, watu 80 katika jimbo la Eastern Cape, na wengine 64 katika jimbo la Free State. Msemaji wa polisi Brigedia Athlenda Mathe amesema maandamano hayo katika mji mkuu wa utawala wa Pretoria yalikuwa ya amani.
Chama cha siasa cha upinzani nchini humo cha Economic Freedom Fighters kilipanga maandamano ya kitaifa Jumatatu, waandamanaji wakiingia barabarani katika miji mikubwa kumshinikiza Rais Ramaphosa kujiuzulu.