Malawi yasema msukosuko wa kipindupindu unaweza kuwa mkubwa zaidi baada ya Kimbunga cha Freddy
2023-03-22 23:05:20| cri

Wizara ya afya ya Malawi imeonya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na hatari kubwa ya kuongezeka kwa wagonjwa wa kipindupindu, kufuatia uharibifu uliosababishwa na Kimbunga cha Freddy ambacho kimeharibu mifumo ya maji na vyoo.

Malawi ilikuwa inapambana na mlipuko mkubwa zaidi wa kipindupindu kuwahi kurekodiwa wakati kimbunga hicho kilipotua wiki iliyopita, na kusababisha maporomoko ya udongo na mafuriko. Kimbunga hicho kimesababisha vifo vya watu 476 na kuwafanya wengine karibu nusu milioni kukosa makazi.

Mlipuko wa kipindupindu ulioanza mwaka jana, umewakumba watu zaidi ya elfu 30 na kusababisha vifo vya zaidi ya 1,700.