Marais wa China na Russia wasisitiza kutatua mgogoro wa Ukraine kupitia mazungumzo ya amani
2023-03-22 09:05:18| CRI

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin jana tarehe 21 katika ikulu ya Kremlin, mjini Moscow walisaini na kutangaza Taarifa ya Pamoja ya Jamhuri ya Watu wa China na Shirikisho la Russia kuhusu Kuimarisha Uhusiano wa Wenzi wa Uratibu wa Kimkakati wa Kina Kwenye Zama Mpya.

Kuhusu suala la Ukraine, pande hizo mbili zimeona kuwa madhumuni na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa lazima zizingatiwe, na sheria za kimataifa lazima ziheshimiwe. Upande wa Russia unapongeza msimamo wa haki na kutopendelea upande wowote wa China kuhusu suala la Ukraine. Pande hizo mbili zinapinga nchi au kundi lolote la nchi kudhuru maslahi halali ya usalama ya nchi nyingine zinapojitafutia manufaa ya kijeshi, kisiasa na mengineyo. Upande wa Russia unasisitiza nia yake ya kurejesha mazungumzo ya amani haraka iwezekanavyo, ambayo China inapongeza. Upande wa Russia unakaribisha kazi zinazofanywa na China za kuhimiza utatuzi wa mgogoro wa Ukraine kwa njia za kisiasa na kidiplomasia, na unakaribisha mapendekezo ya kiujenzi yaliyowekwa kwenye waraka wa "Msimamo wa China juu ya Suluhu ya Kisiasa ya Mgogoro wa Ukraine". Pande hizo mbili pia zilisema ili kutatua mgogoro wa Ukraine, ufuatiliaji halali wa usalama wa nchi zote lazima uheshimiwe na uanzishaji wa makabiliano ya makundi na kuchochea mvutano lazima iepukwe. Pande hizo mbili zilisisitiza kuwa mazungumzo ya kuwajibika ndiyo njia bora ya kutatua matatizo kwa uthabiti. Kwa hivyo, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuunga mkono juhudi zinazofaa za kiujenzi. Pande hizo mbili zimetaka kusitishwa kwa vitendo vyote vinavyochochea mvutano na kurefusha muda wa vita, ili kuzuia mgogoro huo kuwa mbaya zaidi au hata kushindwa kudhibitiwa. Pande zote mbili zinapinga vikwazo vyovyote vya upande mmoja ambavyo havijaidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.