Matokeo ya hojaji ya CGTN yaonyesha hakuna demokrasia uliyo kuu
2023-03-23 15:02:24| cri

Hojaji iliyofanywa na Jopo la Washauri Bingwa la CGTN na Taasisi ya Maoni ya Umma ya Chuo Kikuu cha Renmin cha China imeonyesha kuwa, watu waliohojiwa katika sehemu mbalimbali duniani wanaweka umuhimu mkubwa katika haki za msingi za binadamu kama haki ya kuishi na maendeleo.

Hojaji hiyo imeonyesha kuwa, asilimia 84.8 ya watu waliohojiwa wanaamini kuwa hakuna demokrasia iliyo kuu, na kwamba demokrasia bora ni ile inayoendana na hali ya nchi husika.

Kwa mujibu wa hojaji hiyo, asilimia 84.3 ya watu waliohojiwa duniani wanaamini kuwa hakuna demokrasia moja inayofaa kwa nchi zote, na kwamba demokrasia ina aina tofauti kwa nchi na tamaduni tofauti.

China daima imekuwa ikisisitiza kuwa demokrasia sio pambo la kutazamwa, lakini ni chombo cha kukabiliana na masuala yanayofuatiliwa na watu. Katika miongo iliyopita, China imeboresha kwa kina ujenzi wa mchakato mzima wa demokrasia ya watu, na kutimiza matarajio mapana na endelevu kwa idadi kubwa ya watu.

Asilimia 88.3 ya watu waliohijiwa wanaamini kuwa demokrasia inapaswa kuwa njia ya viongozi wa serikali kuridhia matakwa ya watu, kuhudumia watu, na kuwa tayari kuwajibishwa na watu.