Rais wa China kuufanya ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja uangaze dunia nzima
2023-03-23 15:01:59| cri

Machi 23, 2013, Rais Xi Jinping wa China alitaja kwa mara ya kwanza dhana ya Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja alipotoa hotuba kwenye Chuo cha Mahusiano ya Kimataifa cha Moscow nchini Russia.

Katika miaka 10 iliyopita, Rais Xi kwa nyakati tofauti na sehemu tofauti alitoa mara nyingi pendekezo la kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja. Dhana hiyo imeendelea kurutubika na kukua katika uzoefu halisi, na kutoa uzoefu  na ufumbuzi wa China katika kukabiliana na  mabadiliko ya dunia, zama na historia, na hivyo kuonesha uwajibikaji wa China.
Kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja sio kazi ya upande mmoja, na bali ni ujenzi wa pamoja chini ya mashauriano, na ujenzi wake hauwezi kukamilika kwa hatua moja, bali unahitaji juhudi endelevu. Kujenga jumuiya hiyo ni lengo jema, ambalo linahitaji juhudi za kizazi baada ya kizazi.

Kama alivyosema Rais Xi Jinping, “China itatoa busara ya China, ufumbuzi wa China na nguvu ya China, katika kusukuma mbele ujenzi wa dunia yenye amani ya kudumu, usalama kwa wote, ustawi wa pamoja, na iliyo wazi, shirikishi, safi na nzuri. Tuufanye ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja uangeze dunia nzima!”