Bunge la Ethiopia lakiondoa chama cha TPLF katika orodha ya ugaidi
2023-03-23 09:03:26| CRI

Baraza la Wawakilishi la Ethiopia jana lilikiondoa chama cha ukombozi wa watu wa Tigray (TPLF) katika orodha ya ugaidi.

Baraza hilo ambalo liliingiza rasmi TPLF katika orodha ya makundi ya kigaidi mwezi Mei mwaka 2021, liliamua kuiondoa kwenye mkutano wake maalumu uliofanyika jana.

Hata hivyo baadhi ya wabunge wameeleza wasiwasi wao kutokana na uamuzi huo, na kuhoji utayari wa chama cha TPLF wa kuwa mtekelezaji amani kwenye mchakato wa nchi hiyo.

Waziri wa sheria wa Ethiopia Gedion Timothewos aliwaambia wabunge kuwa chama hicho kimechukua hatua nyingi nzuri za kuhimiza amani, na huo ndio msingi wa uamuzi wa kukiondoa kwenye orodha hiyo.