Rwanda na Uganda zafanya mkutano kutathmini maeneo ya ushirikiano
2023-03-23 09:04:36| CRI

Tume ya 11 ya Pamoja ya Kudumu JPC kati ya Rwanda na Uganda ilikutana jana mjini Kigali, Rwanda kujadili maeneo ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili jirani, ukiwa mkutano wa kwanza wa aina hiyo tangu uhusiano wao kurejea kuwa wa kawaida.

Akifungua mkutano huo, mkurugenzi mkuu wa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda Bw. Shakilla Umutoni amesema mkutano huo wa siku tatu unaashiria kwamba pande zote mbili zimejitolea katika juhudi zinazoendelea za kufufua uhusiano na kuimarisha uaminifu.

Tume hiyo ilifufuliwa mwezi Septemba mwaka 2022 wakati wa mkutano kati ya maafisa wakuu wa serikali ya Uganda na Rwanda nchini Uganda.

Mkutano huo pia utajadili maeneo ambayo juhudi zaidi zinahitajika ili kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya pamoja.