Waziri Mkuu wa Ethiopia amteua afisa mwandamizi wa TPLF kuwa mkuu wa serikali ya mpito ya jimbo la Tigray
2023-03-24 09:16:54| CRI

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia imetoa taarifa ikisema Waziri Mkuu Abiy Ahmed jana Alhamis alimteua afisa mwandamizi wa Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) Getachew Reda, kuwa mkuu wa serikali ya mpito ya jimbo la Tigray.

Kwa mujibu wa taarifa, mkuu wa serikali ya mpito anapewa majukumu ya kuanzisha serikali jumuishi, pamoja na kuongoza na kuratibu bodi ya utendaji itakayoweza kuhakikisha uwakilishi wa watendaji wote wa kisiasa wanaofanya kazi jimboni Tigray. Uteuzi huo umekuja siku moja baada ya Baraza la Wawakilishi kuiondoa TPLF kwenye orodha ya makundi ya ugaidi.