Mtaalamu wa Tanzania: Wanaozungumzia vibaya mfumo wa demokrasia wa China ni kutokana na wivu wa mafanikio ya mfumo huo kwa China
2023-03-24 10:45:06| CRI

Mkutano wa Pili wa Baraza la Kimataifa kuhusu “Demokrasia: Thamani ya Pamoja ya Binadamu Wote” umefanyika tarehe 22 hadi 23 Machi mjini Beijing.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii na Uchumi kati ya Afrika na China kutoka Tanzania Profesa Humphrey Moshi alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) alisema, demokrasia inatakiwa kuzingatia mambo matatu, ambayo ni masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, mambo ambayo China imeyazingatia kwa kikamilifu. Pia amesema, mfumo wa demokrasia wa China ni tofauti na nchi za magharibi, ambao unaleta manufaa mengi, na kusababisha uchumi wa China kukua kwa kasi na kuwa shirikishi. Ameongeza kuwa, wanaouzungumzia vibaya mfumo wa demokrasia wa China ni kwa sababu ya mafanikio makubwa ya China katika uchumi, jamii na siasa.

Profesa Moshi pia ameeleza kuwa, kila nchi ina aina yake ya demokrasia, na haikubaliki kulazimisha nchi nyingine kutumia mfumo wa demokrasia wa nchi moja. Amesema nchi zina hali tofauti za kitaifa, tamaduni na mchakato wa maendeleo, na hakuna mfumo wa kidemokrasia unaofaa kwa dunia nzima.

Amesisitiza kuwa Demokrasia inatakiwa kufuata kiwango kinachoendana na historia, utamaduni na uchumi wa nchi.