China inapenda kujenga uhusiano na Honduras kwa usawa na kuheshimiana
2023-03-24 09:20:25| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Wang Wenbin amesema kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja ni mwelekeo mkuu wa haki wa kimataifa na China inakaribisha tamko chanya lililotolewa na serikali ya Honduras kuhusu kuendeleza uhusiano na China, na inapenda kujenga na kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwenye msingi wa usawa na kuheshimiana.

Bw. Wang alisema hayo jana alipojibu swali kuhusu ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Honduras nchini China.

Kuhusu hoja iliyotolewa na mamlaka ya kisiwa cha Taiwan kwamba Honduras iliwahi kuiomba itoe msaada wa dola za kimarekani bilioni 2.5, na mamlaka hiyo ilishuku kuwa China bara iliunga mkono dai hilo la Honduras, Wang Wenbin alisisitiza kuwa kauli hizi ni za kipuuzi kabisa na hazina msingi.

Wang alibainisha hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje wa Honduras Reina alisema katika mahojiano kwamba uamuzi wa Rais Castro wa kuendeleza uhusiano na China unalingana na mwelekeo mkuu wa dunia na pia ni uamuzi unaozingatia hali halisi ya Honduras yenyewe.