Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimetangaza kuwa, timu ya wataalamu itapelekwa nchini Tanzania ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Marburg (MVD).
Tangazo hilo limetolewa baada ya Wizara ya Afya nchini Tanzania kutangaza jumatatu mlipuko wa kwanza wa ugonjwa huo katika wilaya ya Bukoba, mkoa wa Kagera, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, ambao umesababisha vifo vya watu watano, huku wengine watatu wakiendelea na matibabu.
Africa CDC imesema, nchi mbili wanachama wa Umoja wa Afrika, Guinea ya Ikweta na Tanzania, zimetangaza mlipuko wa MVD.