China na Honduras zaanzisha uhusiano wa kibalozi
2023-03-27 07:46:33| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang jana, mjini Beijing, alifanya mazungumzo na mwenzake wa Honduras Eduardo Enrique Reina, na kusaini taarifa ya pamoja kuhusu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

Honduras, ikiwa nchi muhimu katika Amerika ya Kati, imechagua kushirikiana na nchi 18 duniani, kukubali na kufuata sera ya kuwepo kwa China moja, na kukatiza uhusiano wa kiserikali kati yake na Taiwan, kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Jamhuri ya Watu wa China, na kuahidi kutokuwa na uhusiano wowote wa kiserikali na Taiwan.

Qin Gang amesema, China inapenda kuimarisha ushirikiano na Honduras katika sekta mbalimbali kwa kufuata kanuni tano za kuishi kwa pamoja kwa amani, ili kunufaisha nchi hizo mbili na wananchi wao.