Xi atuma barua ya pongezi kwa Kongamano la Maendeleo la China 2023
2023-03-27 14:39:17| cri

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa Kongamano la Maendeleo la China (CDF) 2023 lililofunguliwa jana Jumapili mjini Beijing chini ya kauli mbiu ya “Ufufukaji wa Uchumi: Fursa na Ushirikiano”.

Rais Xi amesema kwenye barua hiyo kuwa hivi sasa mabadiliko makubwa ambayo hayajashuhudiwa katika karne moja yanaongezeka kote duniani, migogoro ya kikanda na misukosuko vinatokea mara kwa mara, huku ufufukaji wa uchumi wa dunia ukidorora. Ameongeza kuwa kuwezesha kuimarika kwa uchumi wa dunia kunahitaji makubaliano na ushirikiano.

Rais Xi pia amesema, Pendekezo la Maendeleo Duniani GDI lililotolewa na China limepata kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, na kwamba China itaendelea kutekeleza sera yake ya msingi ya kitaifa ya kufungua mlango, kufuata mkakati wa kunufaishana, na kuendelea kuunda fursa mpya kwa dunia kupitia maendeleo mapya ya China.