Uganda yaandaa siku ya kutotumia magari katika mji mkuu ili kukabiliana na uchafuzi wa hewa
2023-03-27 20:39:53| cri

Uganda jana ilitekeleza siku ya kutotumia magari katika mji wa Kampala ikiwa ni jitihada za kupunguza utoaji moshi wa magari na hewa chafu.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mkuu wa Kampala David Luyimbazi, amesema nusu ya mji huo, ambao una wakazi zaidi ya milioni moja, ulizuia matumizi ya magari na kufunguliwa tu kwa watembea kwa miguu na waendesha baiskeli. Alisema Kampala ni moja ya miji duniani yenye hali mbaya zaidi ya uchafuzi wa hewa, hivyo wanatarajia kwa kuwa na siku ya kutotumia magari wataweza kupunguza kiwango cha uchafuzi wa hewa.

Aliongeza kuwa wanajaribu kulinda mazingira dhidi ya moshi wa magari ambao unahatarisha ubora wa hewa, pia wanajitahidi kuhakikisha hewa isiwe na uchafuzi wa kemikali zinazosababisha magonjwa ya mapafu.