Waziri mkuu wa China kuhudhuria mkutano wa mwaka wa Baraza la Asia la Boao
2023-03-27 20:16:15| cri

Waziri mkuu wa China Bw. Li Qiang anatarajiwa kuhudhuria na kutoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka 2023 wa Baraza la Asia la Boao utakaofanyika tarehe 30 mkoani Hainan, China.

Waziri mkuu wa Singapore Bw. Lee Hsien Loong, wa Malaysia Bw. Anwar bin Ibrahim, wa Hispania Bw. Pedro Sanchez, wa Cote d’Ivoire Bw. Patrick Achi na mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bibi Kristalina Georgieva wamealikwa kuhudhuria mkutano huo wa mwaka.

Mbali na kuhudhuria mkutano huo, Bw. Lee Hsien Loong, Bw. Anwar na Bw. Sanchez pia watafanya ziara rasmi nchini China.