Athari mbaya za ukoloni na utumwa bado zinaonekana nchini Marekani
2023-03-28 08:26:19| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Mao Ning amesema, athari mbaya zinazotokana na ukoloni na utumwa bado zinaonekana nchini Marekani.

Mao Ning amesema hayo katika Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Wahanga wa Utumwa na Biashara ya Utumwa kuvuka Bahari ya Atlantiki, inayoadhimishwa Machi 25 kila mwaka.

Mao amesema, kuondoa aina zote za ubaguzi, na kuhakikisha usawa wa utu na haki kwa wote ni kiini cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa na pia kunaonesha haki na usawa wa kimataifa, lakini ubaguzi wa rangi, na ukosefu wa usawa bado umekithiri katika baadhi ya nchi.

Mao Ning amesisitiza kuwa, nchini Marekani athari za ukoloni na utumwa bado zinaendelea hadi leo, na kwamba Marekani inapaswa kutekeleza wajibu wake wa kimataifa wa haki za binadamu, kushughulikia masuala yake ya ubaguzi, huku ikiacha kuingilia kati masuala ya ndani ya nchi nyingine na kuharibu utulivu wa nchi nyingine.