Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema, mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliotokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) unatishia maisha ya zaidi ya watu milioni 1 waliopoteza makazi yao.
Ofisi hiyo imesema, mlipuko huo uliotokea mkoa wa Kivu Kaskazini, umeathiri zaidi maeneo ya Goma, Karisimbi, Masisi na Nyiragongo yanayohifadhi zaidi ya watu milioni 1 waliokimbia makazi yao, na kuongeza kuwa, tangu Machi 13 hadi 19, mamlaka za afya zimerekodi kesi 1,800 zilizothibitishwa na kushukiwa kuwa na ugonjwa huo.