Watu 7 wauawa katika mlipuko uliotokea nchini Afghanistan
2023-03-28 08:34:08| cri

Polisi wa Afghanistan wamesema, watu 7 akiwemo mshambuliaji wameuawa katika mlipuko ulitokea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kabul.

Msemaji wa polisi wa Afghanistan Bw. Khalid Zadran amesema, mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijaribu kufanya shambulizi katika wilaya ya pili ya kipolisi mjini Kabul, ambapo askari waliokuwa karibu na eneo hilo walimshambulia kwa risasi, lakini alilipua bomu alilovaa na kuua watu 7 akiwemo yeye mwenyewe, na kujeruhi wengine kadhaa.

Mpaka sasa, hakuna shirika lolote lililodai kuhusika na shambulizi hilo.