Zaidi ya watu 16 wafariki katika maporomoko ya udongo katikati mwa Ecuador
2023-03-28 08:33:43| cri


 

Sekretarieti ya Usimamizi wa Majanga ya Kitaifa ya Ecuador imesema, watu 16 wamefariki na wengine 16 kujeruhiwa, huku wengine 7 hawajulikani walipo kufuatia maporomoko ya udongo kutoka mlimani yaliyotokea jumapili jioni katika wilaya ya Alausi, mkoa wa Chimborazo nchini humo.

Sekretariet hiyo imesema, maporomoko hayo yalisababisha mita 150 za barabara kuharibika na nyumba 163 kubomoka.

Serikali imetenga sehemu ya hifadhi ya muda kwa waathirika wa maporomoko hayo.