China yatoa ripoti kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Marekani kwa mwaka 2022
2023-03-28 14:44:11| cri

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imetoa ripoti kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Marekani kwa mwaka 2022, na kusema katika mwaka huo kulikuwa na kudorora kwa haki za binadamu nchini Marekani.

Ripoti imesema Marekani inayojitaja kuwa ni “mtetezi wa haki za binadamu” ina magonjwa sugu kama vile siasa za fedha, ubaguzi wa rangi, mabavu ya bunduki na polisi, na pengo kubwa sana kati ya matajiri na maskini.

Ripoti imeongeza kuwa sheria za haki za binadamu zimeshuhudia kurudi nyuma, na kukandamiza haki za kimsingi na uhuru wa watu wa Marekani.