Watoto weusi wakumbwa na hatari zaidi ya kushambuliwa kwa bunduki nchini Marekani katika kipindi cha COVID-19
2023-03-29 18:33:46| cri

Kutokana na utafiti ulionukuliwa na shirika la habari la WHYY, mashambulizi ya bunduki yaliyotokea katika miji minne ya Marekani yameongezeka maradufu kwa vikundi vyote vya kijamii katika kipindi cha COVID-19, lakini watoto weusi walikuwa kwenye hatari zaidi ya kuwa wahanga. Utafiti unasema watoto weusi walikuwa na uwezekano wa mara 100 zaidi wa kushambuliwa kwa bunduki ikilinganishwa na watoto wazungu.

Tofauti hiyo iliongezeka zaidi katika kipindi cha COVID-19. Kwa mujibu wa utafiti huo, kuanzia Machi 2020 hadi Desemba 2021, watoto 34 weusi kati ya laki moja walikuwa walishambuliwa kwa bunduki, ikilinganishwa na watoto 0.34 kati ya watoto laki moja wazungu.