Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimezindua vifaa muhimu vitakavyosaidia ufuatiliaji wa bara hilo dhidi ya magonjwa ya mlipuko katika siku zijazo.
Kaimu Mkurugenzi wa Afrika CDC Ahmed Ogwell Ouma amesema, vifaa hivyo ni pamoja na mpango kazi na kadi ya kuweka rekodi ili kutathmini bila upendeleo uwezo wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kutekeleza mifumo ya tahadhari ya mapema na majibu dhidi ya mlipuko wa magonjwa.
Naye kaimu mkuu wa Idara ya Usimamizi na Uelewa wa Magonjwa iliyo chini ya Africa CDC Yenew Kebede amesema, bara hilo lina uhitaji mkubwa wa mfumo wa mapema wa tahadhari za afya kwa kuwa linakabiliwa na changamoto kubwa katika kudhibiti milipuko ya magonjwa.