Umoja wa Afrika wataka mshikamano urejee Kenya wakati biashara nchini humo zikipata hasara kubwa kila siku
2023-03-29 23:32:56| cri

Mashirika mbalimbali ya kimataifa na ya kienyeji yametoa wito kwa viongozi wa Kenya kuingia kwenye mazungumzo wakati maandamano yanayoendelea nchini humo yakisababisha hasara ya kibiashara kufikia hadi shilingi bilioni 3 kwa siku.

Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Faki Mahamat, ameeleza wasiwasi wake kuhusu ghasia hizo nchini Kenya kufuatia maandamano ya kuipinga serikali yaliyoanza tarehe 20 mwezi huu, akitaka wadau wote nchini humo kuwa na utulivu na kuingia kwenye mazungumzo kushughulikia tofauti zao kwa maslahi ya mshikamano na maridhiano ya kitaifa.