China yapinga kinachoitwa “mtego wa madeni” ya China
2023-03-29 08:40:18| cri


 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Mao Ning amesema, migogoro mingi na uhaba wa chakula zimesababisha hatari ya madeni ya nchi zinazoendelea kuongezeka hivi karibuni.

Akizungumza na wanahabari jana, Mao Ning amesema, kutokana na hilo, baadhi ya watu wametunga kile kinachoitwa “mtego wa madeni” ya China, na kuichafua China, jambo ambalo China halikubaliani nalo. Amesema China siku zote inafanya juhudi kuunga mkono maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi zinazoendelea, na kuongeza kuwa, China siku zote inashikilia kanuni ya uwazi, na kufanya ushirikiano wa uwekezaji na kukusanya fedha pamoja na nchi zinazoendelea.