Watu 39 wafariki katika ajali ya moto kwenye mpaka wa Mexico
2023-03-29 08:35:41| CRI

Mamlaka ya Uhamiaji ya Mexico imesema, watu 39 wamefariki na wengine 29 kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali ya moto iliyotokea usiku wa jumatatu katika kituo cha wahamiaji iliyoko mjini Ciudad Juárez, Jimbo la Chihuahua, nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo imesema, moto ulianzia eneo la makazi ndani ya kituo hicho, na mamlaka ya uhamiaji imezitaka idara zinazohusika kufanya uchunguzi.

Habari zinasema, kituo hicho kiko karibu na daraja la mpakani kati ya Mji wa Ciudad Juárez na Marekani, na wakati ajali hiyo inatokea, kulikuwa na wahamiaji 68 ndani ya kituo hicho.

Rais wa Mexico Andrés Manuel López ametangaza kuwa, ajali hiyo imetokea baada ya wahamiaji walioko kwenye kituo hicho kuambiwa kuwa watarejeshwa nchini kwao, ambapo walijifungia ndani na kuwasha moto.