Kituo cha habari cha CMG nchini Honduras chazinduliwa Tegucigalpa
2023-03-29 15:31:58| cri

Kituo cha habari cha Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG nchini Honduras kimezinduliwa rasmi Machi 28 mjini Tegucigalpa.

Hafla ya uzinduzi ilifanyika kwenye Ikulu na kuhudhuriwa na maofisa mbalimbali waandamizi, watu wa sekta ya habari na utamaduni wa nchi hizo mbili wakiwemo waziri wa habari wa Honduras Bw. Ivis Alvarado na mkuu wa makao makuu ya CMG katika Latin Amerika Bw. Zhu Boying.

Ofisi ya habari ya Ikulu ya Honduras ilituma barua ya pongezi kwenye uzinduzi wa kituo cha habari cha CMG nchini humo, na kusema hatua hii itajenga daraja la urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.